Maelezo ya jumla

Tutakuwa tunasoma tunda la Roho. Hata hivyo,sio kuangalia tunda tu bali dhambi zetu nyingi za mwili ambazo hupigana na tunda la Roho. Lengo lako nikusaidia wanafunzi wako kuwa mabingwa. Kufanya hivi, hawafai tu kuelewa mistari ya kukariri na kujifunza hadithi za Biblia, lakini wanahitaji pia kuweka tunda la Roho kwenye vitendo katika maisha yao ya kilasiku.

"Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. " Wagalatia 5:22-23

Kitengo cha 1

Somo la 1

Upendo dhidi ya ubinafsi
Hadithi ya Biblia: Yesu afa msalabani
Mathayo 27:27-56

Mstari wa kukariri:

"Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu. "
1 Yona 3:16

Ndani ya Uwanja

Cheza mchezo ambao marafiki wako wanapendekeza,cheza wakati ambao watataka(kama una ruhusa)na ucheze kwa muda wowote mabao wanataka.usiwatajie ule mchezo unataka kucheza.wakati huu,mahitaji yako hayajalishi,kwa sababu unaonyesha mapenzi ya ukweli bila mawazo yoyote kwako.

Somo la 2

Upendo dhidi ya mtazamo wa kuhukumu watu
Hadithi ya Biblia: Kibanzi na boriti
Mathayo 7:1-5

Mstari wa kukariri:

“Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa. "
Mathayo 7:1-2

Ndani ya Uwanja

Ambia mtu “kazi nzuri” na pongezi kwao kwa kitu mzuri ambacho unaona.kuja na kioo ndogo ya mfuko na ushinde nayo siku mzima.wakati unajaribiwa kuhukumu mtu,chukua kioo cha mfuko na ujiangalie.jikumbukushe yakuwa hufai kusaidia wengine kurekebisha makosa yao.

Somo la 3

Upendo dhidi ya chuki
Hadithi ya Biblia: Yuda amuuza Yesu
Mathayo 26:14-16

Mstari wa kukariri:

"Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona. "
1 Yona 4:20

Ndani ya Uwanja

Fanya kitu kizuri kwa mtu ambaye hupendi. Zuia ulimi wakati unaona mtu mwingine akidanganya ama akiwa karibu kufanya kitu kibaya. Usiwaingize kwenye shida.

Somo la 4

Upendo dhidi ya kujihalalisha
Hadithi ya Biblia: Mfano wa msamaria mwema
Luka 10:25-37

Mstari wa kukariri:

“Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.”
Luka 10:27

Ndani ya Uwanja

Simama kusaidia mtu ambaye ako na shida,kupuuza visingizio vyote unaweza kuwa nazo vya kutosaidia.fanya kitu maalum kwa mtu ambaye hayuko kwenye kiwango chako cha jamii..

Somo la 5

Upendo dhidi ya ubatili wa kiroho
Hadithi ya Biblia: Daudi kuchaguliwa kama mfalme
1 Samuel 16:1-13

Mstari wa kukariri:

"Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. "
1 Wakorintho 13:4-7

Ndani ya Uwanja

Uliza Mungu kama kuna zoezi la kiroho ambalo unafaa kuacha,huku ukielekeza lengo lako kwa UPENDO. Fanya vitendo hii wiki kuonyesha upendo:usiringe,fanya kile ambacho nicha kusaidia wengine,na usiwajibishe watu kwa makosa ambayo wanafanya.

Somo la 6

Furaha dhidi ya Wivu
Hadithi ya Biblia: Viongozi wa dini wana wivu
Matendoya mitume 5:12-33

Mstari wa kukariri:

"kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu? "
1 Wakorintho 3:3

Ndani ya Uwanja

Shukuru Mungu kwa vipawa vya kiroho,muonekano wa nje,milki zako,na familia ambayo uko nayo. Uliza Mungu akupe furaha na ridhaa ambayo unayo.chagua mtu ambaye unaweza kuwa unaweza kuwa aliona wivu hapo mbeleni na umpe zawadi ndogo.(usiwaambie kuhusu wivu wako wa kitambo)

Somo la 7

Furaha dhidi ya ulafi
Hadithi ya Biblia: Kijana tajiri
Mathayo 19:16-30

Mstari wa kukariri:

“Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.”
Luka 12:15

Ndani ya Uwanja

Mpe Mungu baadhi ya pesa yako ya kibinafsi kama sadaka kwa kanisa,bila kujua inaendea nani,tumia baadhi ya pesa yako kutumikia mtu. Kama huna pesa yoyote,chukua unachomiliki naupeane.

Somo la 8

Furaha dhidi ya kujihurumia
Hadithi ya Biblia: Yona na mdudu
Yona 4:1-10

Mstari wa kukariri:

"Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi. Mtu asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima. "
2 Wakorintho 4:17-18

Ndani ya Uwanja

nyumba ya wasio na makazi, ama huduma ambayo inawapa chakula maskini.njia ingine, tembelea maskini katika hospitali.omba na uulize Mungu akufungue macho katika picha ile kubwa,na akusaidie utoe macho ya kujiangalia mwenyewe.

Somo la 9

Furaha dhidi ya kukosa shukrani
Hadithi ya Biblia: Yesu aponya watu kumi wenye ukoma
Luka 17:11-19

Mstari wa kukariri:

"Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake; "
Zaburi 100:4

Ndani ya Uwanja

Shukuru wazazi wako(ama mtu mwingine)kwa kitu ambacho wao hukupa kila siku.chagua kitu uende bila kwa muda, kama ukumbusho yakuwa huwezi kuwa nacho kila wakati.

Somo la 10

Amani dhidi ya Hofu
Hadithi ya Biblia: Eliya alishwa na kunguru
1 Wafalme 17:1-6

Mstari wa kukariri:

"Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa."
Mathayo 6:33

Ndani ya Uwanja

Gawa kitu ambacho unacho na mtu mwingine,atakama inamaanisha itabidi ukae bila. Iwe ni chakula,nguo,nauli ya basi,ama kitu chochote ambacho kitakugharimu pesa. Uliza Mungu atimize mahitaji yako.

Somo la 11

Amani dhidi ya woga
Hadithi ya Biblia: Petro atembea juu ya maji
Mathayo 14:22-33

Mstari wa kukariri:

"Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]”
Mathayo 17:20-21

Ndani ya Uwanja

Chagua kitu ambacho kinahisi kama haiwezekani,na uweke uwoga kando. Uliza Bwana Yesu akusaidie kufanya. Kisha anza hatua ndani yake.(ni fanikio kwako kwanza, atakama utazama kama vile Petro alizama.kazi nikuchagua kitu ambacho unahisi nikama haiwezekani na kukijaribu)

Somo la 12

Amani dhidi ya ugomvi
Hadithi ya Biblia: Geuza shavu hilo lingine
Mathayo 5:38-42

Mstari wa kukariri:

"Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. "
Warumi 12:18

Ndani ya Uwanja

Jiruhusu ufanyiwe kitu kibaya mara moja hii wiki.(uwezekano Zaidi itafanyika yenyewe)kazi yako ya ziada ni kutofanya lolote.

Somo la 13

Amani dhidi ya Imani ya kibinafsi
Hadithi ya Biblia: Yesu awapa chakula watu 5000
Luka 9:10-17

Mstari wa kukariri:

"Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. "
2 Wakorintho 12:9

Ndani ya Uwanja

Uliza Mungu nafasi umtumikie pahali ambapo huna nguvu. Ingia kwenye kanisa na umtumikie huko. Kama umekimya,ongea Zaidi hii wiki. Kama uko na kelele Nyingi,kuwa wa kunyamaza hii wiki.

 

 

Kitengo cha 2

Somo la 1

Uvumilivu dhidi ya kukosa uvumilivu
Hadithi ya Biblia: Ndama ya dhahabu
Kutoka 32

Mstari wa kukariri:

"mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha" Wakolosai 1:11

Ndani ya Uwanja

Andika kwenye sakafu kile Mungu amekufanyia samani katika siku za nyuma, kisha weka jiwe kama doa la alama. Fanya moja kanisani, kila mwanafunzi akifanya doa lao maalumu, na kufanya lingine nyumbani wakati wa wiki. Baada ya kuweka jiwe doa ya alama yako, shiriki na mtu mwingine kile Mungu alifanya.

Somo la 2

Uvumilivu dhidi ya Huzuni
Hadithi ya Biblia: Ayubu anateseka na uvumilivu
Ayubu 1-2

Mstari wa kukariri:

"Hii ndiyo faraja yangu katika
taabu yangu, Ya kwamba ahadi yako imenihuisha."
Zaburi 119:50

Ndani ya Uwanja

Andika asante kwa Mungu juu ya jambo ambapo uliteseka. Jaribu kusema kama alivyofanya Ayubu, "Bwana alitoa, na Bwana ametwaa. Jina la Bwana lisifiwe.” Shiriki na wengine katika darasa ushuhuda wako kama unaweza.

Somo la 3

Uvumilivu dhidi ya Kiburi
Hadithi ya Biblia: Mfalme Nebukadreza
Danieli 4

Mstari wa kukariri:

"Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake, Na mvumilivu rohoni kuliko mwenye roho ya kiburi." Mhubiri 7:8

Ndani ya Uwanja

Fanya shughuli kadhaa kujinyenyekeza. Unaweza kumpa mtu nafasi yako katika mstari, epuka kutazama kipinda katika runinga ambapo wahusika wamejaa kiburi, peana sehemu yako katika jukwaa au mbele ya wengine, au ruhusu wengine kuwa sahihi.

Somo la 4

Uvumilivu dhidi ya Hasira
Hadithi ya Biblia: Daudi, Nabali na Abigaili
1 Samweli 25

Mstari wa kukariri:

"Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka..." Waefeso 4:26

Ndani ya Uwanja

Nunua vitu vichache vidogo upeane kama zawadi. Wakati unapokuwa na hasira, toa bidhaa kwa mtu uliye na hasira naye. Jaribu kupoteza hasira yako kwa kutoa zawadi ndogo kwa watu, na kutazama jinsi uvumilivu wako unavyo kua.

Somo la 5

Uvumilivu dhidi ya Haki
Hadithi ya Biblia: Manna na kware
Kutoka 16: 1-18

Mstari wa kukariri:

"Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia. Ndugu, msinung'unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango."
Yakobo 5: 8-9

Ndani ya Uwanja

Wiki hii hudaiwi na mtu chochote. Kila wakati unataka kuomba kitu, jizuie mwenyewe. Kila wakati unapo jizuia mwenyewe kutoka kuomba chakula, kibali, wakati, au msaada; unapata ushindi dhidi ya dhambi hii.

Somo la 6

Wema dhidi ya Kulinganisha
Hadithi ya Biblia: Mfalme Sauli na Daudi
1 Samweli 18: 5-16

Mstari wa kukariri:

"Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake."
Wagalatia 6:4

Ndani ya Uwanja

Jipatie mwenyewe mipira midogo 20 mwanzoni mwa wiki. Kila wakati unapo jipata ukijilinganisha na wengine, ondoa mpira moja. Hii ni pamoja na facebook au vifaa mengine kwenye mtandao ambapo sisi mara nyingi hujilinganisha na wengine. Kama inahitajika, funga facebook kwa wiki nzima.

Somo la 7

Wema dhidi ya Udanganyifu
Hadithi ya Biblia: Petro amkana Kristo
Mathayo 26: 31-35, 69-75

Mstari wa kukariri:

"Sikuketi pamoja na watu wa ubatili, Wala sitaingia mnamo wanafiki."
Zaburi 26:4

Ndani ya Uwanja

Wiki hii, enda kwa mtu ambaye ulimdanganya, na uwaambie ukweli. Omba msamaha kwa uongo, na uombe wakusamehe. Kila wakati unaporudi na kusema ukweli itakuwa ushindi mwingine mkubwa dhidi ya dhambi hii.

Somo la 8

Ukarimu dhidi ya kujiondoa
Hadithi ya Biblia: Ruthu na Naomi
Ruthu 1: 8-22

Mstari wa kukariri:

“Usiwanyimewatu mema yaliyo haki yao,Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda.”
Mithali 3:27

Ndani ya Uwanja

Tafuta mtu wa kumsaidia, hasa kama "sio tatizo lako." Mpe mtu asiye na makao, au labda mtoto katika shule anayehitaji kalamu mpya au Raba. Hakikisha kuwa hawana husiano na wewe, na kwamba huna wajibu au haja ya kuwasaidia.

Somo la 9

Ukarimu dhidi ya Uovu Fitina
Hadithi ya Biblia: Esta aokoa watu wake
Esta 3-5

Mstari wa kukariri:

"Ndugu zangu, nimehakikishwa mimi mwenyewe kwa habari zenu ya kuwa ninyi nanyi mmejaa wema, mmejazwa elimu yote, tena mwaweza kuonyana."
Warumi 15:14

Ndani ya Uwanja

Linda mtu wiki hii kutokana na mtu anayewakosea bila sababu. Tunapo linda mtu mwingine, pia tunakabiliana na dhambi hii katika mioyo yetu wenyewe. Hatarisha sifa yako mwenyewe kwa kulinda mtu mwingine.

Somo la 10

Wema dhidi ya kutojali
Hadithi ya Biblia: Sodoma na Gomora
Mwanzo 18: 16-33

Mstari wa kukariri:

"Kwake huyo atakaye kuzima roho inapasa atendewe mema na rafiki; Hata kwake huyo aachaye kumcha
Mwenyezi."
Ayubu 6:14

Ndani ya Uwanja

Omba na umuulize Mungu ili akuongezee shauku katika moyo wako wiki hii. Tafuta kitu unachoweza kufanya kwa wengine ili uongeze shauku yako kwa wengine. Tembelea huduma fulani na ujifunze kuhusu kile wanachokifanya, saidia katika makazi yanayolisha watu wengine, au tazama video kuhusu mahitaji yalio duniani. Husika mahali uwezavyo.

Somo la 11

Uzuri dhidi ya Uovu
Hadithi ya Biblia: Herode na Yohana
Luka 3: 18-20, Mathayo 14: 1-12

Mstari wa kukariri:

"Uache mabaya ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie."
Zaburi 34:14

Ndani ya Uwanja

Tazama karibu nawe uwepo wa uovu, ambapo mtu anaumiza mwingine bila sababu. Tafuta njia ya kuingilia kati wiki hii ili ulinde mtu asiye na hatia. Labda umsaidie atembee njia tofauti kwenda nyumbani kutoka shuleni, mpe chakula cha mchana, au kuwa na kundi la watu 4 wajiunge na wewe katika kutembea pamoja.

Somo la 12

Wema dhidi ya Jitihada za Ubinafsi
Hadithi ya Biblia: Mnara wa Babeli
Mwanzo 11: 1-9

Mstari wa kukariri:

"Msitende neno lo lote kwa
kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake."
Wafilipi 2:3

Ndani ya Uwanja

Usifanye lolote wiki hii ili uongeze umaarufu wako au kujulikana. Kila wakati nafasi ikitokea, kataa. Unapofanya hivyo, utakuwa unapiga ngumi dhambi hii jeuri.

Somo la 13

Wema Dhidi ya Uchafu
Hadithi ya Biblia: Yusufu na Potifa
Mwanzo 39: 1-21

Mstari wa kukariri:

"Kwa hiyo twawaombea ninyi sikuzote, ili Mungu wetu awahesabu kuwa mmekustahili kuitwa kwenu, akatimiza kila haja ya wema na kila kazi ya imani kwa nguvu"
2 Wathesalonike 1:11

Ndani ya Uwanja

Linda moyo wako wiki hii. Kama kuna kitu umetendewa dhidi yako, kumbuka kwamba wao ndio waliokosa, sio wewe. Sema katika maombi kila siku, "Mimi ni safi mbele yako, Mungu". Kama umefanya kitu dhidi ya mtu mwingine, omba msamaha kwa mtu huyo na pia Mungu. Kisha unaweza kuomba, "Mimi ni msafi mbele yako, Mungu."

 

 

Kitengo cha 3

Somo la 1

Uaminifu dhidi ya Ibada ya sanamu
Hadithi ya Biblia: Sanduku linatekwa
1 Samweli 5: 1-12, 6, 7: 3

Mstari wa kukariri:

"Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia."
Kutoka 20:4

Ndani ya Uwanja

Chagua shughuli ambaye HUWEZI kushiriki katika sababu inaweza kuwa na ibada ya sanamu. Inaweza kuwa ni desturi kuondoa viatu vyako, gwaride ya kutoshiriki katika, mchezo wa kutohudhuria, au kukosa kununua maua wakati wengine wanafanya hivyo.

Somo la 2

Uaminifu dhidi ya Uhaini
Hadithi ya Biblia: Shadraka, Meshack na Abednego
Danieli 3: 1-21

Mstari wa kukariri:

"Ee Bwana, unifundishe njia yako; Nitakwenda katika kweli yako; Moyo wangu na ufurahi kulicha jina lako."
Zaburi 86:11

Ndani ya Uwanja

Tafuta nafasi wiki hii kusema waziwazi shuleni au katika jamii kuwa wewe ni Mkristo, na kwamba unaamini Yesu Kristo. Baada ya hapo, furahia kwamba umekuwa mwaminifu na kikundi kidogo, licha ya shinikizo yoyote unakabili.

Somo la 3

Uaminifu dhidi ya Kusita
Hadithi ya Biblia: Bwana anamwita Samueli
1 Samweli 3: 1-21

Mstari wa kukariri:

"Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana."
Waebrania 11:1

Ndani ya Uwanja

Mwombe Mungu azungumze nawe wiki hii, na akuelekeze kufanya kitu fulani. Fanya mazoezi ya kutii mara moja bila kusita. Kama utasahau na kusubiri, uliza Mungu akupe zoezi jingine.

Somo la 4

Uaminifu dhidi ya Kutotii
Hadithi ya Biblia: Wapelelezi katika kanaani
Hesabu 13: 1-3,17-33, 14: 1-11

Mstari wa kukariri:

"Musa akawaambia, Kwa nini ninyi sasa kuyahalifu maagizo ya Bwana? Maana halitafanikiwa jambo hilo.!"
Hesabu 14:41

Ndani ya Uwanja

Chagua zoezi 2 kutoka kwa Mungu kufanya wiki hii. Ya kwanza iwe ni jambo Mungu alikuuliza USI fanye, na kingine Mungu alikuuliza ufanye. Mtii Mungu katika mambo yote mbili ili kushinda dhidi ya uasi.

Somo la 5

Uaminifu dhidi ya kuzuia
Hadithi ya Biblia: Ibrahimu na Isaka
Mwanzo 22: 1-18

Mstari wa kukariri:

"Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao."
Waebrania 11:6

Ndani ya Uwanja

Je, kuna kitu ambacho Mungu anakuuliza kuachana naye wiki hii? Chukua muda kufi kiria ni nini hio, na kisha kuomba kwamba Mungu akupe nguvu kuachana kwa muda. Inaweza kuwa chai, Facebook, au chakula unaependa. Ili kushinda vita hii, chagua kuachana na jambo hilo wiki mzima.

Somo la 6

Uaminifu dhidi ya kutoaminika
Hadithi ya Biblia: Nuhu na Safina
Mwanzo 5:32, 6: 1-22, 7: 1-12

Mstari wa kukariri:

"Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu."
Yakobo 2:18

Ndani ya Uwanja

Chagua eneo la maisha yako ya kuaminika kwa Mungu. Chagua jambo la kufanya kwa Mungu siku moja wiki hii, na kuhakikisha kuaminika ndani yake. Baada ya kumaliza, chagua ahadi nyingine kwa Mungu kwa siku, na kuweka siku gani ya kufanya hivyo. Hakikisha kukamilisha ahadi yako.

Somo la 7

Uaminifu dhidi ya Mashaka
Hadithi ya Biblia: Yesu anamtokea Tomaso
Yohana 20: 24-31

Mstari wa kukariri:

"Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki."
Yohane 20:29

Ndani ya Uwanja

Chagua kuamini Mungu wiki hii juu ya jambo ambalo aliahidi na inaonekana haiwezekani.
Mwambie Mungu kuwa uko tayari kusubiri mpaka tamati ya ahadi. Ili kuonyesha nia yako ya kusubiri, nenda usimame katika mstari yoyote, kile ambalo huna haja ya kuwa! Andika ni dakika ngapi ulisubiri katika mstari ili uweze kuripoti kwa kocha yako.

Somo la 8

Upole dhidi ya Mgawanyiko
Hadithi ya Biblia: Ibrahimu na Lutu wagawana
Mwanzo 13: 1-18

Mstari wa kukariri:

"kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo."
Waefeso 4:2

Ndani ya Uwanja

Ruhusu mtu mwingine kushinda wakati hamkubaliani juu ya jambo fulani. Unaweza chagua kutokubaliana, lakini jizuie mwenyewe kutoka kupambana juu yake. Waruhusu kuwa na maoni yao.

Somo la 9

Upole dhidi ya Mila
Hadithi ya Biblia: Safi na chafu
Mathayo 15: 1-20

Mstari wa kukariri:

"Msiwakoseshe Wayahudi wala Wayunani wala kanisa la Mungu, vile vile kama mimi niwapendezavyo watu wote katika mambo yote, nisitake faida yangu mwenyewe, ila faida yao walio wengi, wapate kuokolewa."
1 Wakorintho 10: 32-33

Ndani ya Uwanja

Chagua wema kwa mtu kuliko mila yako. Hii inamaanisha kuelewa wakati wanavunja mila yako, na bila kutoa maoni kuhusu hilo. Hakikisha usi umize mtu mwingine, au kuchukua tahadhari kwako mwenyewe na zoezi hili.

Somo la 10

Upole dhidi ya Uchungu
Hadithi ya Biblia: Caini na Abeli
Mwanzo 4: 1-16

Mstari wa kukariri:

"Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondok kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya."
Waefeso 4:31

Ndani ya Uwanja

Chagua mtu uliye na hasira nao, na uasamehe. Chukua muda katika maombi, na kusema kwa sauti kubwa, "Mimi nimekusamehe."

Somo la 11

Kiasi dhidi ya Majaribu
Hadithi ya Biblia: Yesu anajaribiwa
Mathayo 4: 1-11

Mstari wa kukariri:

"Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili."
1 Wakorintho 10:13

Ndani ya Uwanja

Pinga jaribu moja, na kama unaweza, tumia andiko kama Yesu alivyofanya. Dumisha udhibiti wa tamaa yako, na wala usiruhusu mwenyewe kufungulia jaribu hilo.

Somo la 12

Kiasi dhidi ya Kudanganya
Hadithi ya Biblia: Yakobo anaiba Baraka za Esau
Mwanzo 27: 1-36

Mstari wa kukariri:

"limi unenao uongo huwachukia wale uliowajeruhi; Na kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu."
Mithali 26:28

Ndani ya Uwanja

Kila mtu anasema uongo, hata kama wengine tu ni kidogo. Kumbuka hapo nyuma uongo ulisema mwaka huu. Nenda kwa mtu huyo, waambie ukweli, na kuwaambia pole kwa uongo.

Somo la 13

Kiasi dhidi ya Uvivu
Hadithi ya Biblia: Wajenzi wenye busara na wapumbavu
Mathayo 7: 24-27

Mstari wa kukariri:

"Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi."
Yakobo 4:17

Ndani ya Uwanja

Pambana dhidi ya uvivu yako wiki hii, kwa kuchagua kitu cha kufanya ambaye hutaki kufanya. Hakikisha kukamilisha hayo, na kushirikisha ushuhuda wako na rafi ki.