Mipango

VBS Rahisi

Karibu kwa "Mwelekeo bila mipaka" VBS rahisi ambaye ni rahisi kupanga na rahisi kufanya. Chukua tu tarehe, kukusanya baadhi ya watu wa kujitolea, hegemesha baadhi ya mabango kuzunguka jamii, na utakuwa tayari kwenda!

Mwaka huu, timu katika "Watoto ni wa muhimu" walitembelea VBS kadhaa katika nchi mbalimbali na kuona mabadiliko gani ya mitaala makanisa wangependa. Baadhi ya makanisa nchini India wakaomba shughuli ZAIDI kwa muda mrefu ikitumiwa na watoto katika VBS. Kwa sababu hii, tumeongeza vituo mbili zaidi, Kituo cha misioni, na kituo cha Biblia ambapo yusufu anakuja kutembelea! Yatakuwa vituo rahisi kufanya, itaongeza furaha zaidi na mafunzo kwenye VBS yako, na kukupa maudhui zaidi kwa VBS kama inavyohitajika.

Ombi lingine ilikuwa kwa ajili ya shughuli zaidi kwenye karatasi za wanafunzi. Tuna furaha kubwa kwamba tumeweza kujumulisha shughuli 5 mbalimbali kwenye 1/2 ya kipande cha karatasi! Hii inapaswa kutoa zaidi kwa wanafunzi wako kufanya, kwa gharama ndogo sana kwa kila mtoto.

Ukitumia mfumo wa "mzunguko", au mfumo wa kawaida "darasani", kuna mengi zaidi za shughuli ya kufanya VBS yako kusisimua, ambapo kanisa lote litajifunza pamoja jinsi ya "kupata maisha yao kwa kupoteza.

Michezo za kuigiza

Michezo za kuigiza ni njia za furaha kuanzisha somo kila siku, kama vile kuwasaidia wanafunzi kuunganisha mafundisho maishani yao ya kila siku. Tunapendekeza kutumia waigizaji walel wale kila siku, na kwamba wao wabaki na vazi hizo wiki yote. Wanaweza kutembelea vituo na kusalimia wanafunzi, na kuchukua pichja za "selfies” na wanafunzi nasibu siku mzima.

Katika Michezo za kuigiza mwaka huu, sungura anajifunza kuteleza na ski, na kongoni ni mwalimu wake. Lengo ni kwenda njia yote hadi kilele na Ski kutoka huko, lakini sungura kwanza lazima kuanza kwenye mteremko chini na njia rahisi ili kuteleza vizuri. Katika kila mchezo wa kuigiza, sungura lazima kujifunza somo sawa ambaye watoto wanajifunza. Sababu sungura atakuwa anaporomoka na kuanguka katika baadhi ya Michezo, ajiri kijana au mwana riadha muigizaji kwa sungura ikiwezekana.

Mfumo wa msunguko wa VBS

VBS hii imeandikwa kutumika na mzunguko ratiba na vituo tatu kwa wakati. Hii ina maana kwamba utaweka kundi lako katika makundi matatu, na makundi hayo yatazunguka kupitia vituo za shughuli tatu. Kila kituo huchukua muda wa dakika 20 hadi 40, na kila kituo inarudiwa mara tatu ili kila kundi linakwenda kila kituo mara moja kila siku..

Njia rahisi ni kugawanya kundi lako katika makundi za umri moja mara tatu ambaye tunatumia kwa ajili ya kurasa zetu za wanafunzi:

  • Rahisi (umri wa miaka 4-6)
  • Kati (umri wa miaka 7-9)
  • Ngumu (umri wa miaka 10-12)

Tunapendekeza kwamba utumie vijana (miaka 13+) kama wasaidizi wadogo kwa VBS yako. Hata hivyo, kurasa "ngumu” za wanafunzi itakuwa ya furaha kwa miaka yote ya wakubwa, ikiwa ni pamoja na watu wazima. njia yetu tunayependa ni mzunguko kupitia vituo ni kucheza muziki wakati wa mzunguko, hivyo kwamba wanafunzi wana nguvu ya mzunguko kutoka kituo kimoja hadi kingine.

Mfumo wa kawaida darasani

Kama badala yake huwezi tumia ratiba ya mzunguko, kuna ratiba na mfumo wa kawaida darasani kwa VBS yako. Ratiba hii ina faida ya kuchukua muda zaidi, kama unahitaji VBS ndefu. Hata hivyo, inahitaji walimu wengi zaidi, sababu kila kundi umri inahitaji Yusufu muigizaji, pamoja na walimu ambao watajifunza shughuli zote mbalimbali.

Wafanyakazi

Pamoja na timu kubwa ya wafanyakazi, VBS ni furaha zaidi kwa kila mtu anayeshiriki, hivyo tumegawanya kazi katika majukumu mbalimbali ili kuhusisha watu wengi zaidi. Majukumu yafuatayo ya wafanyakazi yamo kama utatumia mfumo wa mzunguko:

Mkurugenzi wa VBS 1
Kiongozi wa nyimbo 1 (Waziada kusaidia kwa vitendo vya nyimbo)
Muhubiri kwa somo kuu 1
Waigizaji wa mchezo wa kuigiza 2 (Kongoni na Sungura)
Viongozi kwa vikundi vidogo vidogo 6, Viongozi wa kila umri 2. (Wana kwenda na wanafunzi kwa vituo mbalimbali)

Vituo :
Kituo cha Biblia 2 (Mratibu 1, Muigizaji 1 wa Yusufu)
Mratibu wa Darasa 1 (kwa karatasi ya Shughuli za wanafunzi)
Mratibu wa Ufundi 1
Mratibu wa vinywaji 1
Mratibu wa Michezo 1
Mratibu wa Misheni 1

Ratiba ya kawaida (masaa 6)

Ufunguzi wa saa ya kundi (masaa 1 1/2)
Dakika 30 Ibaada: Tumia somo kuu kwa kila siku
Dakika 30 Nyimbo: Tumia nyimbo zenu mnazopenda za kuabudu pamoja na CD mpya zinazotolewa maalum kwa ajili ya VBS hii.
Dakika 15 Mchezo wa kuigiza ya Kongoni na Sungura (husaidia kuanzisha mada ya siku)
Dakika 15 Pitia mada kuu ya siku, kumbukumbu kuu la mstari ya siku, kisha tenganisha katika madarasa
Saa ya Darasani (masaa 1 1/2)
Dakika 15 Fanya shughuli za darasa na Yusufu (kutoka kituo cha Mlima wa Biblia)
Dakika 15 Kufanya shughuli darasani na Yusufu (kutoka kituo cha Mlima wa Biblia)
Dakika 45 Karatasi za shughuli za wanafunzi (kutoka kituo cha darasa la ski)
Dakika 15 Shughuli za Kupiga kura (kutoka kituo cha darasa la ski)
Wakati wa vinywaji / Chai (dakika 30) (kutoka kituo cha mgahawa wa kilele)
Wakati wa Darasani (masaa 1 1/2)
Dakika 20 Jifunze kuhusu misheni (kutoka kituo cha safari za kimishenari)
Dakika 30 Shughuli za Misheni (kutoka kituo cha safari za kimishenari)
Dakika 40 Muda za ufundi (kutoka kituo cha kibanda cha ufundi)
Wakati wa Michezo (dakika 30) (kutoka kituo cha michezo ya barafu)
Wakati wa kundi Kufunga (dakika 30)
Dakika 15 Nyimbo
Dakika 15 Tathmini na matangazo kwa ajili ya kesho