The Bridge LogoUpangaji

VBS Ambayo ni Rahisi

 Mkononi mwako umeshika VBS ambayo ni rahisi, rahisi kupanga na ni rahisi kutumia. Chukua tu tarehe, kusanya baadhi ya watu watakao jitolea, Weka baadhi ya mabango ya mwaliko katika maeneo yalio na jamii, na utakuwa tayari kwenda!

Ukiwa na timu kubwa ya wafanyikazi, VBS ina raha zaidi kwa kila mtu ambaye atakaye husika, kwa hivyo tumeamua kugawanya hii kazi kwa vitengo kadhaa na majukumu ambayo yata husisha watu wengi.

Hapa tuna baadhi ya mawazo kwa ajili yako ili uweze kugawanya mzigo wa kazi ya VBS yako:
Mkurugenzi 1 mkuu wa VBS.
Kiongozi 1 wa Nyimbo.
Mhubiri 1 wa somo kuu.
Waigizaji 2 kwenye mchezo wa kuigiza (nahodha na roboti).
Mratibu 1 wa darasa (vitabu vya wanafunzi na marudio ya somo).
Mratibu 1 wa ufundi.
Mratibu 1 wa vitafunio.
Mratibu 1 wa michezo
Viongozi 6-10 wa kila kundi ndogo, kulingana na idadi ya watoto kwenye VBS yako.

Michezo ya kuigizaBlast Off! Galaxy Express

Kila siku nahodha ataongoza watoto kwenye safari ndani ya meli ya anga “Galaxy Express” kwa usaidizi wa naibu wake roboti.
Nahodha wenu ni mtu wa kumaanisha sana kwani ana jukumu la kuongoza meli hii, pia ana jukumu la kuhakikisha kuwa watoto wamepata upokezo wa kiroho katika wiki hiyo. Anatambulisha msaidizi wake roboti kwa watazamaji: Anakaa machachari na saa zingine roboti huyu hafanyi kazi viruzi, Wakati mwingine roboti hunong’ona anapoongea, anaishia kunongo’na kutema nje sauti zisizo eleweka badala ya maneno. Kila wakati anahitaji mafuta kwenye viungo vyake ili aweze kuendelea kusonga.
Kila siku nahodha na roboti watawasilisha hoja kuu ya siku hiyo, na jinsi watoto wanavyo paswa kuitikia   kila wakati wanapoisikia.  Nahodha pia atawasilisha sehemu ya kutenda watoto watakayosikia katika vikundi vyao vidogo.
Mawazo ya michezo ya kuigiza yanatolewa kwenye ufunguzi wa kila siku, lakini pia unaweza funga siku nayo, au uwe na wahusika wakushiriki katika michezo au enda ukizunguka na utembelee madarasa. Watoto watapenda kupata kujuana na nahodha na roboti!

Changamfu, katika Utendaji!

Kila siku, wanafunzi watajifunza usemi mmoja wa ile siku, na kuitikia kwa vitendo. Hii shughuli ni muhimu sana ili wanafunzi wako wasipate kuchoka wakati wa mahubiri makuu, na hii itafanya VBS yako yote maalum. Katika VBS mzima, wakati wowote kiongozi anataja usemi wa siku, wanafunzi wanafaa kuwa wanajua jinsi ya kuitikia na tendo linalo ambatana nao. Watajifunza wakati wa mchezo wa kuigiza na nahodha pamoja na roboti, na unaweza kutumia somo hili siku ile yote.

Message Relay Galaxy ExpressKupashana Ujumbe

Safari ya kwanza

Wakati wa somo hili, kila wakati wanafunzi wanaposikia "Mwite Mungu," ruhusu waitikie kwa kusema: "Bwana, Nisaidie!" Huku wakiruka na kuinua mikono yote miwili kuelekea kwa Mungu.

Message Relay Galaxy ExpressKupashana Ujumbe

Safari ya pili

Wakati wa somo hili kila mara wanafunzi wanapo sikia haya maneno “Itikia kwa Mungu ‘wafanye wajibu kwa kusema “Ndio Bwana” huku wakiweka mikono yao kwa sikio. Kisha wanagongesha miguu yao pamoja kama askari huku wakisema “hapa nipo!”.

Message Relay Galaxy ExpressKupashana Ujumbe

Safari ya tatu

Kila wakati wanafunzi wanaposikia "Mtii Mungu" wakati wa somo, ruhusu wanafunzi kujibu kwa kusema " Mimi lazima nisonge mbele " huku wakisimama na kubadilishana viti na wanafunzi wengine.

Message Relay Galaxy ExpressKupashana Ujumbe

Safari ya nne

Kila wakati wanafunzi wakisikia "Ngojea Mungu" wakati wa somo, wanafunzi wajibu kwa kusema "Niko tayari" huku wakiruka juu na kufanya ndondi, na kisha kusema "lakini mimi lazima kusubiri" wakiweka mikono yao pamoja na kukaa chini.

Message Relay Galaxy ExpressKupashana Ujumbe

Safari ya tano

Kila wakati wanafunzi wakisikia "Mwabudu Mungu" wakati wa somo, wanafunzi wajibu kwa kusema "Ninakuabudu" huku waki inua mikono yao juu katika anga na kukitikisa mbele na nyuma.

GamesMichezo

Michezo katika hii ratiba  itachezwa  na  watoto  wote  wakiwa wameketi  kwenye  kikundi  kikubwa  na kugawanywa  kwa  timu kadhaa (unaweza  kuwa  na timu 2-4.)  Kwa urahisi iwe ni kati ya wavulana dhidi ya wasichana. Kwa  kila  mchezo  kila  timu   itatuma  watu wachache ambao watajitolea  kuwakilisha  timu  zao  na  wengine watakuwa   wakisaidia wenzao ambao wanacheza  kwa kupiga mayowe, kushangilia  na  kucheka  kutoka  kwa  viti vyao. Ili watoto wasichoke kila wanapo cheza, wanafaa wachezeshwe michezo mbalimbali tofauti kila siku, kila mchezo utakua una chukua muda mfupi huku wakibadilisha wachezaji wengine wanaojitolea kushiriki kwenye mchezo.
Wazo moja kwa ajili ya kuchagua wanafunzi ambao watashiriki kwanza katika mchezo , ni kwa kuangalia vizuri wanafunzi wenye tabia jema wakati wa shughuli zingine za VBS yako. Wape wanafunzi hawa kitu kitakachoonyesha kuwa watapata kushiriki kwenye michezo. Inaweza kuwa kitu kinachoninginia shingoni mwao, kitu kinachofungwa katika mkono wao au kadi ambayo wata iweka mfukoni mwao.
Kwa kila mchezo, jinsi unavyo fanya matayarisho kabambe kabla ya wakati wa michezo, ndivyo michezo     itakavyo kuwa ya kufana zaidi kwa wanafunzi wa VBS yako. Utakapokua unajitayarisha katika hii michezo,  fikiria “michezo ya maonyesho ” au “ Nickelodeon”  vipindi  vya maonyesho katika runinga .Unaweza kua na vitambaa ambavyo vinang’aa na vitavaliwa na  wanafunzi ambao watakuwa kwenye   mstari wa mbele, na pia sauti athari au muziki  wakati wa  mchezo , na pia unaweza kuweka mapambo.
(Tumepeana wimbo utakao chezwa wakati wa michezo ambao utachezwa kwenye CD ya Galaxy Express.)
Mnaweza fanya vitu vya gharama ya chini ambavyo vitaongeza furaha katika VBS yenu. Kwa hivyo kueni tayari kuwa na raha na furaha!

Schedule Galaxy Express Sunday SchoolMpangilio

(2½-Ratiba ya saa)
Mwanzo wa nguvu!
(Nyimbo-dakika 20
Mchezo wa wakuigiza wa ufunguzi-dakika 10)
Dharula kutoka Udhibiti wa Misheni ….
(Somo kuu & Mstari wa kukariri-dakika 20)
….kwenye vituo
Ukumbi wa maamkuli (kituo cha vitafunio & utendaji katika anga.
Uhandisi (Kituo cha Ufundi)
Darasa la Kadeti (Vitabu vya wanafunzi na kituo cha marudio)
…..kurudi kwa daraja….
Michezo ya Angani
(Michezo-dakika 30)
Kadeti waondoke.
(Wimbo wa kufunga & Matangazo-dakika 10)

Vituo vya Mzunguko

Katikati  mwa kila siku watoto watawanyika katika vikundi vitatu ambavyo watazunguka  katika vituo   hivyo: Ukumbi wa  maamkuli  ( kituo  cha  vitafunio na utendaji katika anga), uhandisi  (ufundi) na  darasa  la  kadeti (vitabu  vya  wanafunzi  na  marudio ya somo). Soma mengi kuhusu vituo kwenye ukurasa ufuatao.

Mess Hall Station Galaxy ExpressChumba cha maamkuli

Kituo cha Vitafunio

Hapa utapata maagizo jinsi utakavyo tayarisha vitafunio. Weka kwa mawazo kua wanafunzi wanaweza furahia kwa kuunda vitafunio kama ufundi kabla ya kuvila. Usikose fursa ya kuwafunza wanafunzi wako jinsi ya kujifanyia usafi wenyewe baada ya kumaliza kupika vitafunio.

Factoid Galaxy ExpressWazo-(Utendaji katika anga kujadiliwa wakati wa kula vitafunio)
Wakati  wakula  vitafunio,  jadiliana na wanafunzi kuhusu  utendaji katika  anga  na jinsi inavyo ambatana katika somo na  maisha ya wanafunzi ya kila siku. Taarifa kuhusu vitafunio na utendaji katika anga zina patikana kwenye kijitabu cha kiongozi katika ukumbi wa maamkuli.

Engineering Station Galaxy ExpressUhandisi

Kituo cha ufundi

Hapa utapata wazo la ufundi, pamoja na mapendekezo na maelekezo ya vifaa hivyo. Vifaa vyote vya ufundi vinavyo patikana ndani ya Galaxy Express kwenye ratiba ya VBS vimebuniwa kutumia angalau karatasi moja kwa kila ufundi, hii inasaidia kwa kupunguza gharama iwezekanavyo. Kwenye tovuti una weza kutoa mifano, na pia utafute maelezo kuhusu ufundi kwenye mwongozo wa mkurugenzi na pia kwenye kijitabu cha viongozi wa uhandisi.  Pia utapata mifano ya kutoa nakala kwenye kijitabu cha Uhandisi.

Cadet Class Galaxy ExpressDarasa la Kadeti

Vitabu vya wanafunzi na kituo cha marudio

Hapa utapata maelezo ya baadhi ya maneno muhimu kutoka kwa hadithi za bibilia katika lugha ya ishara. Rudia hadithi hio huku ukifunza kwa lugha ya ishara. Kisha peana vitabu vya wanafunzi na umsaidie yeyote ambaye ana maswali.  Habari hii pia inaweza patikana kwenye kijitabu cha kiongozi wa darasa la kadeti.

Familia
Vidole gumba na kidole cha pili yakigusana, Fanya mzunguko wa nje hadi mikono igusane.
Family in Sign Language