Kustahimili Msituni VBS

Chukua darubini na mfuko wako wa safari na kuabiri gari aina ya jeep, kwa sababu ni wakati wa VBS ya msituni! Dunia inayotuzunguka ni kama msitu, ambapo tunajifunza namna ya kustahimili ingawa wengine wanajaribu kututumia ili kujinufaisha, kutuibia, au kutupumbaza. Hata hivyo, tunaweza kuwa wajasiri wakati tunapogundua sini ni nani katika Yesu Kristo. "Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; Na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu. "Waebrania 12: 1 Kama msitari wa mada yetu unavyosema, tunahamasishwa na wale waliotutangulia ili nasi tuwe na ujasiriwa kushinda hofu, dhambi, na mashambulizi ya aina yoyote. Katika VBS hii tutakwenda katika safari ya ndani msituni, na kutokea upande wa pili tukitambua kuwa sisi ni sehemu ya familia ya Mungu, tukiwa na ujasiri, wema, ridhia na nguvu!

Mafunzo

(Kiingereza)